TOP 10 AMAZING PLACES TO SPEND YOUR HOLIDAY THIS DECEMBER TANZANIA

TOP 10 AMAZING PLACES TO SPEND YOUR HOLIDAY THIS DECEMBER TANZANIA

Ni nini kinachofanya sehemu iwe nzuri kwa ajili ya Fungate?

Kwa kweli inategemea utu na nia ya wachumba. Wengine wanpenda sehemu iliyotulia na kuna wengine wanapenda kukaa mjini na kujifunza historia ya mji.

Kwa bahati nzuri, karibia chochote unachokitaka utakipata Tanzania. Kwa kuwa kuna ufukwe vya kutosha, mbuga za wanyama, hoteli za nyota 5 na watu wazuri, ni nchi nzuri ya kuanza maisha mapya na mpenzi wako.

Kukuanzisha, pitia orodha yetu ya sehemu kumi za kimapenzi za kutembelea kwa ajili ya fungate Tanzania. Zitafanya wewe na mpenzi wako muendeleze hisia zenu za kimapenzi zaidi na zaidi.

1. Lazy Lagoon Island Lodge, Bagamoyo

Lazy Lagoon iko kusini mwa Bagamoyo na ni sehemu nzuri sana kwa wachumba wanaopenda kuwa kwenye fukwe binafsi pamoja na huduma ya kipekee.Bagamoyo inaumbali wa lisaa limoja kutoka Dar es Salaam na inachukua dakika 15 kufika Lazy Lagoon kutoka Bagamoyo mjini.

2. Nungwi, Zanzibar

Image result for Nungwi, Zanzibar

Kama unataka fungate ufukweni na yenye huduma ya hali ya juu kabisa, basi Nungwi iliyopo kaskazini mashariki ya Zanzibar, ndio pakwenda.

Kuna malazi mengi mazuri Nungwi na Hideaway of Nungwi Resort & Spa ni mojawapo. Ina vyumba ambazo zinamfaa mfalme (zipitie hapa), spa, huduma za kuchua na za urembo, gym na mengineyo. Hii ni sehemu ya kwenda kama unataka kupumzika kama wafalme.

3. Mullers Mountain Lodge, Usambara

Related image

Kama hamtaki kwenda kwenye fungate ufukweni ila bado mnataka kufurahia mazingira ya kimapenzi, basi malazi yaliopo ndani ya milima ya Usambara yatakuwa suluhisho.

Mullers Mountain Lodge ina banda zilizojengwa kwa mitindo ya zamani lakini zenye vifaa vya kisasa. Pia, unaweza kutembea kwenye milima hizo na zipo karibu na mporomoko wa maji. Zinaleta mazingira za kinyumbani zaidi na zimekuwepo kwa zaidi ya miaka 10. Wanajua namna ya kukusaida kupumzika na vilevile kuhakikisha unaondoka na kumbukumbu safi.

4. Uroa, Zanzibar

Image result for Uroa, Zanzibar

Hotelihii ya gharama nafuu ina huduma za kuvutia ambazo sio gali sana. Huduma maalum zinazotolewa ni pamoja na:

 • Mlo wa jioni ya kibinafsi karibu na bwawa la kuogelea likitazama Bahari wa Hinfi
 • Matembezi ya bahari kwa kutumia boti. Utakuwa na wavuvi watakao kupeleka kwenye ziada ya aina yake baharini mpaka kwenye miamba ya matumbawe
 • Michezo ya majo kama scuba diving, snorkeling na kite surfing.

5. Bushtops Camp, Serengeti

Related image

Hakuna mtu aliyesema kwamba mapenzi hayawezi kuchangamshwa. Tembelea mbuga ya wanyama bora duniani na mpenzi wako.

Kati ya kambi zote zilizopo Serengeti, Bushtop Campus ndio bora kwa wachumba. Chakula chao ni cha kufurahia sana, ina vifaa vya kisasa na wanyama bora. Inasemekana kuwa ni eneo bora ya mbuga za wanyama duniani.

6. The Palms, Bwejuu

Image result for The Palms, Bwejuu

Gazeti maarufu ya Travel + Leisure iliichaguwa The Palms kama moja kati ya hoteli za mapumziko bora duniani. Kama unataka kuishi kifahari na pesa sio tatitizo, hapa patakufaa.

The Palms ina villa 6 tu za kipekee zeilizopambwa na rangi na fenicha za kisasa za kizanzibari. Pia, zina:

 • Bwawa la kuogelea
 • Dstv na DVD player
 • Bar ndogo
 • Bar inayotoa huduma za chain a kahawa
 • Sehemu ya kuhifadhi vitu muhimu
 • Simu
 • AC

Zaidi ya hapo, kuna migahawa, bar, spa, michezo ya maji na vinginevyo vya kufurahia. We na mchumba wako hamtaboreka kabisa.

7. Mount Meru Game Lodge na Sanctuary, Arusha

Image result for Mount Meru Game Lodge na Sanctuary, Arusha

Hoteli iliyopo kati ya mto na eneo ya wanyamapori, imetulia. Mandhari yake ni kitulivu na unaweza ukakutana na pundamlia, mbuni, nyani na mengineyo. Ni sehemu nzuri sana kwa wachumba wanaotaka kupata uzoefu wa kuona wanyama pamoja na utamaduni.

Kuna vyumba 15, 2 zikiwa Suite za kifahari amabazo zina sebule, chumba cha kulala pamoja na sehemu ya kuota moto. Suite hizi pia zina bustani na baraza zao.

Mambo mengine yakufanya ni:

 • Kwenda kwenye ziada ya kahawa
 • Kwenda kwenye matembezi ya utamaduni na elimu
 • Kucheza Golf
 • Kwenda kununua shanga.

8. Malaika Beach Resort, Mwanza

Image result for Malaika Beach Resort, Mwanza

Ukifikiria mtazamo wa kuvutia wa maji kwenye sehemu ya kwenda kwenye Fungate, wengi wetu tutafikiria Zanzibar. Ila Mwanza, ambapo Ziwa Victoria ilipo, pia ina mengi ya kuvutia. Pia, ni masaa mawili kutoka upande wa Magharibi ya Serengeti na pia kuna  Rubondo Island National Park. Kwa hiyo, unaweza kufurahia mitazamo mizuri ya Ziwa Victoria pamoja na kuangalia wanyama.

9. Pole Pole Bungalows, Visiwa vya Mafia

Related image

 

Kama unataka kwenda sehemu ya kuwa na mchumba wako kwa muda maalum bila kusumbuliwa, Visiwa vya Mafia zina mchanganyiko mzuri wa utulivu na uzuri wa ajabu zitakazo kusaidia kufurahia muda wako na mpenzi wako.

Pole Pole Bungalows zinatumia asili ya Visiwa vya Mafia kutengeneza mazingira ambayo hutakuja kusahau.

10. Protea Hotel Courtyard, Dar es Salaam

Image result for Protea Hotel Courtyard, Dar es Salaam

Kama unataka fungate ya mjini zaidi iliyojaa na mitoko mbalimbali, basi Dar es Salaam ndio pakwenda. Kuna migahawa mizuri yenye vyakula vya nyumbani/kiasili, pamoja na vya nje vikiwemo vya Ethopia, Italia na China. Pia, kuna baa nyingi zenye bendi, utalii wa kitamaduni, hoteli zilizopo ufukweni pamoja na visiwa vya kutembelea. Kwa kifupi, huweza ukaboreka

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *